Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 3: Familia > Lesson 4: Bibi na babu

    

BIBI NA BABU (GRANDMOTHER AND GRANDFATHER)

Babu na bibi ni kiungo muhimu cha familia. Wao wanasaidia kulea watoto na kuwafundisha maadili ya maisha.

Bibi anawasaidia wajukuu wake kukatakata mikate, kumimina chai na kuweka sukari.

Wajukuu wanajifunza tabia njema za kula na hasa kula kwa mikono kwa sababu ni desturi yao.

Chakula ni sehemu muhimu katika kuonyesha uhusiano wa kindugu na kifamilia. Familia hukaa pamoja na hula pamoja. Desturi hii ni muhimu kwa familia zote za kiafrika.

 

 

 

© African Studies Institute, University of Georgia.