Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 3: Familia > Lesson 5: Kutembeleana

    

KUTEMBELEANA. TO VISIT EACH OTHER

Ni muhimu pia kwa familia kutembeleana. Kitendo hiki kinaimarisha uhusiano baina ya ndugu na marafiki wa familia.

Huyu ni ndugu Josefu. Shemeji yake anamtembelea na sasa wanaamkiana.

Huyu ni mtoto wa ndugu Josefu. Anaanza kujifunza namna ya kuamkia kwa heshima.

Sasa kaka mkubwa wa Joseph anafika na mke wake na watoto wao. Josefu anawakaribisha na kuwaamkia. Halafu wao wanawaamkia watu wote kabla ya kukaa.

Baadaye watoto wanawaamkia wageni kwa heshima. Watoto wanasema “shikamoo” na wakubwa wanajibu “marahaba”.

 

 

 

© African Studies Institute, University of Georgia.