Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 5: Kununua na Kuuza. Buying and Selling > Diagnostic test
Jibu maswali yote
1. Uko dukani. Unataka kununua mahitaji yako ya shule. Unahitaji madaftari, penseli, kalamu, na vifutio. Bei ya vitu hivi ni: daftari moja – shilingi 350; penseli moja – shilingi 55; kalamu moja – shilingi 130. Unataka kununua madaftari matatu, penseli tano, kalamu mbili, na vifutio vine. Andika mazungumzo baina yako na mwuzaji. (You are at a store. You want to buy your school supplies. You need notebooks, pencils, pens, and erasers. The price of these things is: one notebook – 350 shillings; one pencil – 55 shillings; one pen – 130 shillings. You need 3 notebooks, 5 pencils, 2 pens, and 4 erasors. Write a dialogue between you and the seller.)


2. Uko sokonni. Unataka kununua maembe, mchicha, na samaki. Bei ya vitu hivi ni: embe moja – shilingi 100; kifungu kimoja cha mchicha – shilingi 500; kilo moja ya samaki– shilingi 1000. Unataka kununua maembe matano, vifungu vnine vya mchicha, na kilo tatu za samaki.. Andika mazungumzo baina yako na mwuzaji. (You are at the market. You want to buy mangoes, spinach, and fish. The price of these things is: one mango – 100 shillings; 1 bunch of spinach – 500 shillings; one kilo of fish – 1000 shillings. You want to buy 5 mangoes, 4 bunches of spinach, and 3 kilos of fish. Write a dialogue between you and the seller.)


3. Uko katika duka la nguo. Unataka kununua nguo mbali mbali. Uliza bei za nguo hizi na jaribu kupatana bei. Chagua na nunua nguo tatu tofauti. Andika mazungumzo na mwuzaji. (You are at a cloth store. You want to buy different kinds of clothes. Ask for prices and try to bargain. Choose and buy three different kinds of clothes. Write your dialogue with the seller.)


4. Uko posta katika mji wa Dar es Salaam, Tanzania. Unataka kutuma Marekani kifurushi kimoja na kadi za posta mbili. Unataka kujua bei ya kutuma kifurushi na unataka kununua stempu mbili za kadi. Andika mazungumzo baina yako na mfanya kazi wa posta. (You are at the post office in Dar es Salaam, Tanzania. You want to send to the US a parcel and two post cards. You want to know how much it will cost to send the parcel and you want to buy two stamps for the post cards. Write a dialogue between you and the post office clerk).


Instructor's Email:
Your Name:
Your email:

 

© African Studies Institute, University of Georgia.