Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 5: Kununua na Kuuza. Buying and Selling > Lesson 1: Kununua matunda na mboga

 


    

KUNUNUA MATUNDA NA MBOGA (BUYING FRUITS AND VEGETABLES).

Juma na Halima ni majirani. Wao wanakaa Zanzibar. Zuena na Halima huenda sokoni pamoja.

Juma: Hujambo bi Halima?

Halima: Sijambo. Habari za asubuhi?

Juma: Salama tu, nyumbani hawajambo?

Halima: Wote hawajambo.

Juma: Leo wewe unakwenda sokoni kununua nini?

Halima: Mimi ninataka kununua vitu vingi leo. Nitanunua matunda mbalimbali. Ninataka maembe, mapapai, mananasi, na mafenesi. Pia nataka mboga, nitanunua mchicha na kisamvu.

Juma: Vipi utanunua choroko leo?

Halima: Hapana, sitanunua choroko leo, ila nitanunua maharage, na njegere. Wewe utanunua nini?

Juma: Mimi nitanunua matunda. Nitanunua machenza na machungwa. Pia nataka mboga. Nataka bamia na maboga.

Halima:Vipi utanunua viungo leo?

Juma: Nitanunua viungo vichache sana. Ninataka binzari, iliki na mdalasini. Pia Ninataka nyama ya ng’ombe na samaki.

Halima: Leo tutanunua vitu vingi.

 

 

© African Studies Institute, University of Georgia.