Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 5: Kununua na Kuuza. Buying and Selling > Lesson 2: Kununua samaki

    

KUNUNUA SAMAKI. (BUYING FISH).

Hasani na Pili ni majirani. Wao wanakaa Dar-es Salaam. Leo wanakwenda pwani kununua samaki.

Hasani: Hujambo bi Pili?

Pili: Sijambo, habari za leo?

Hasani: Nzuri tu, nyumbani hawajambo?

Pili: Wote wazima. Leo wewe unataka kununua samaki gani?

Hasani: Mimi leo ninataka kununua changu na nguru. Pia ninataka nyama za pwani. Ninataka kamba na kombe. Wewe utanunua papa na pweza?

Pili: Hapana, mimi sitanunua papa na pweza. Watoto wangu hawapendi pweza na mume wangu hapendi papa. Ninataka changu.

Hasani: Haya twende ili tuwahi mnada.

Pili: Sawa, pia tuwahi kupata vijana wa kupaa na kusafisha samaki.

 

 

© African Studies Institute, University of Georgia.