Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 5: Kununua na Kuuza. Buying and Selling > Lesson 3: Kununa nguo

    

KUNUNUA NGUO. (BUYING CLOTHES).

Mwuzaji: Karibu , karibu.

Mteja : Asante.

Mteja: Shati hili kiasi gani?

Mwuzaji: Shilingi elfu tisa.

Mteja: Vipi mzee bei ya shati haipungui?

Mwuzaji: Nipe shilingi elfu nane mia tano.

Mteja: Sawa. Nataka mashati mawili.

Mwuzaji: Sawa mzee.

Mteja: Hii suruali bei gani?

Mwuzaji: Shilingi elfu kumi na mbili.

Mteja: Na hii fulana je?

Mwuzaji: Shilingi elfu tano.

Mteja: Vipi mzee bei haipungui?

Mwuzaji: Nipe elfu nne mia tano kwa fulana na elfu kumi na moja kwa suruali.

Mteja: Sawa, nipe suruali mbili na fulana tatu. Ninataka suruali rangi nyeusi na suruali rangi ya khaki. Ninataka fulana rangi nyeupe, nyekundu na nyeusi.

Mwuzaji: Sawa mzee.

 

© African Studies Institute, University of Georgia.