Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 5: Kununua na Kuuza. Buying and Selling > Lesson 4: Kununua vifaa vya shule

    

KUNUNUA VIFAA VYA SHULE. BUYING SCHOOL NEEDS.

Bi Monika anakaa Kilimanjaro. Yeye ana duka la vifaa vya shule. Duka lake lipo katikati ya mji wa Moshi. Katika duka lake anauza madaftari, vitabu, kalamu, penseli rula, kalamu za rangi n.k. Kwa siku anapata wateja wengi.

Mwuzaji: Karibu, karibu.

Mteja: Asante. Asante.

Mteja: Daftari hili bei gani?

Mwuzaji: Shilingi mia tatu.

Mteja: Na kitabu cha sayansi bei gani?

Mwuzaji: Shilingi elfu moja.

Mteja: Vipi, bei haipungui?

Mwuzaji: Haipungui. Hakuna maslahi.

Mteja: Nataka madaftari saba.

Mwuzaji: Vipi, hutaki kitabu cha sayansi?

Mteja: Hapana mama, leo sina pesa za kutosha.

Mwuzaji: Ahsante mzee.

Mteja: Kalamu za rangi bei gani?

Mwuzaji: Shilingi mia sita.

Mteja: Na rula, bei gani?

Mwuzaji: Shilingi mia mbili.

Mteja: Vipi, bei haipungui?

Mwuzaji: Haipungui mzee.

Mteja: Nipe kalamu za rangi pakti moja na rula tatu.

Mwuzaji: Sawa baba yangu.

 

© African Studies Institute, University of Georgia.