Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 5: Kununua na kuuza. Buying and Selling > Lesson 6: Kutuma barua

    

KUTUMA BARUA KWA REJISTA. (TO SEND REGISTERED MAIL).

Mteja: Bahasha za rejista zipo?

Mhudumu: Eeh zipo.

Mteja: Basi nisaidie moja.

Mhudumu: moja, eh?

Mteja: eh!

Mteja: Na gharama ya kutuma?

Mhudumu: Ngoja tupime. Itakuwa shilingi sabini. Bandika hiyo stempu halafu nipe hiyo rejista. Haya subiri risiti yako.

Mteja: Haya.

Mteja: Sasa hii niipeleke wapi?

Mhudumu: Ah, hii ni risiti yako itabidi ukae nayo mpaka utakapopata jibu kuwa huyo bwana kuwa ameshapata rejista yake.

Mteja: Ah.

Mhudumu:Kwa hivyo itunze vizuri.

Mteja: Sawa. Haya, asante.

Mhudumu: Haya. Karibu.

Mteja: Haya.

 

© African Studies Institute, University of Georgia.