Rehema na Tina ni wanafunzi wa shule ya msingi. Wao wanasoma shule
tofauti. Rehema anasoma
shule ya msingi Mtakuja na Tina anasoma shule ya msingi Miburani.
Juma: Habari za leo Tina?
Tina: Salama tu. Kesho utakwenda shule saa ngapi?
Juma: Nitakwenda saa kumi na mbili asubuhi. Na nitarudi
saa tisa mchana.
Tina: Kwa nini utakwenda shule mapema
sana?
Juma: Kwa sababu tunafanya usafi wa mazingira kabla
ya kuanza masomo. Baada
ya kusafisha mazingira sisi hukaa kwenye baraza, halafu tunaenda
madarasani.
Tina: Sisi pia tunafanya usafi wa mazingira. Kila darasa
lina sehemu yake maalum ya kufanya usafi. Viranja na walimu wa zamu
husimamia usafi wa mazingira na shughuli nyingine.
Juma: Kesho darasa lenu mtasoma masomo gani?
Tina: Sisi tutasoma sayansi, hisabati, Kiswahili, na
jiografia.
Juma: Sisi tutasoma kemia, Kiingereza, baolojia na fizikia.