John na Ali ni wanafunzi wa shule za msingi. John anasoma
shule ya Amani katika mkoa wa Tabora, na Ali anasoma shule ya
Jamhuri, katika mkoa wa Dar-es-Salaam. John na Ali wapo likizo, na wanakutana mkoani
Iringa
John: Hujambo Ali?
Ali: Sijambo, habari za Tabora?
John: Nzuri tu. Habari za Dar-es-Salaam?
Ali: Salama kabisa. Ninyi mmefunga
shule kwa
muda gani?
John: Sisi tumefunga shule kwa muda wa mwezi mmoja, na
ninyi je?
Ali: Na sisi tumefunga kwa muda wa mwezi mmoja. Vipi mitihani
ilikuwaje?
John: Mitihani ilikuwa mizuri tu, nimefaulu vizuri .
Nimekuwa mtu wa
tatu darasani.
Ali: Mimi pia nimefaulu vizuri. Nimekuwa mtu wa pili.
John: Mkifungua shule utaingia
darasa la ngapi?
Ali: Tukifungua shule nitaingia darasa la saba. Na wewe
je?
John: Mimi nitaingia darasa la tano.
Ali: Ninyi shuleni kwenu mnavaa sare
za rangi gani?
John: Wasichana wanavaa mashati
meupe na sketi za bluu, na wavulana wanavaa mashati meupe
na kaptula za bluu.
Ali: Sisi pia tunavaa kama
ninyi.