Hamisi na Rukia ni majirani. Wao ni wanafunzi wa shule za sekondari
. Hamisi na Rukia wanasoma shule tofauti. Rukia anasoma shule ya
sekondari ya wasichana, Kisutu, na Hamisi anasoma shule ya sekondari
ya Jitegemee.
Hamisi: Hujambo Rukia?
Rukia: Sijambo, habari za masomo?
Hamisi: Salama tu.
Rukia: Kesho utakwenda shule saa ngapi?
Hamisi: Nitakwenda saa sita. Wiki hii tunaingia mchana na
wewe je?
Rukia: Nitakwenda saa moja asubuhi. Wiki hii tunaingia
asubuhi.
Hamisi: Wewe unachukua mkondo gani?
Rukia: Mimi ninachukua mkondo wa biashara, na wewe je?
Hamisi: Mimi ninachukua mkondo wa sayansi. Nilitaka
kuchukua mkondo wa sanaa
lakini nimebadilisha
mawazo.
Rukia: Katika mkondo wa sayansi mnasoma masomo gani?
Hamisi: Tunasoma fizikia, baolojia, kemia, hisabati. Pia
tunasoma lugha na jiografia. Ninyi mnasoma masomo gani?
Rukia: Katika mkondo wa biashara tunasoma uhasibu na biashara. Pia
tunasoma lugha, jiografia na baolojia.