Nuru na Kombo ni wanafunzi wa shule za sekondari. Wao wanasoma
mikoa tofauti. Nuru anasoma shule ya bweni ya Mkonge katika mkoa
wa Tanga, na Kombo anasoma shule ya bweni ya Msufini katika mkoa
wa Morogoro. Wao wanakutana Dodoma , wote wapo likizo.
Kombo: Hujambo Nuru?
Nuru: Sijambo Kombo. Habari za Morogoro?
Kombo: Nzuri tu. Habari za Tanga?
Nuru: Salama tu. Vipi mitihani ilikuwaje?
Kombo: Mitihani ilikuwa mizuri. Bado nasubiri matokeo, na
wewe je?
Nuru: Haikuwa mibaya sana, na mimi pia bado nasubiri
matokeo.
Kombo: Mkifungua shule utaingia kidato cha
ngapi?
Nuru: Nitaingia kidato cha nne, na wewe je?
Kombo: Nitangia kidato cha tatu. Vipi uko tayari kwa
masomo ya kidato cha nne?
Nuru: Nipo tayari
kabisa, na nitaanza kujiandaa na mtihani wa
Taifa mara tu tukifungua shule.
Kombo: Vyema, ninakutakia kila
la kheri.
Nuru: Asante.
Kombo:Ninyi shuleni kwenu mnavaa sare za rangi gani?
Nuru: Wasichana wanavaa sketi za kijani na mashati meupe,
na wavulana wanavaa suruali za khaki na mashati meupe.
Kombo: Sisi shuleni kwetu wasichana wanavaa mashati meupe
na sketi nyeusi, na wazulana wanavaa suruali za khaki na mashati
meupe.