Josefu ni mkazi wa Mwanza. Yeye anatembelea
mkoa wa Dar-es-Salaam. Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam kipo katika
mkoa wa Dar-es-Salaam. Mwenyeji wake anamweleza shughuli mbalimbali za
chuo.
Mwenyeji: Karibu bwana Josefu, habari za leo?
Josefu: Nzuri tu. Nimekuja kutembelea chuo chenu.
Mwenyeji: Karibu bwana. Chuo chetu ni kikubwa, kina majengo mengi. Kina ofisi
za walimu, ofisi za idara mbalimbali, mabweni ya wanafunzi,
madarasa, na ukumbi wa mikutano.
Josefu: Asante bwana. Hapa chuoni, lugha ya
kufundishia ni lugha gani?
Mwenyeji: Ni Kiingereza, isipokuwa madarasa ya Kiswahili,
wanatumia Kiswahili.
Josefu: Sawa kabisa. Je na madarasa yanafundishwaje?
Mwenyeji: Ni mchanganyiko wa mhadhara na majadiliano. Mwalimu
anafundisha kwa kuwauliza wanafunzi maswali. Kwa hiyo wanafunzi wanachangia mawazo
yao.
Josefu: Hapa chuoni mnatoa shahada katika nyanja gani?
Mwenyeji: Hapa tunatoa shahada katika nyanja
mbalimbali kama elimu, biashara, uhandisi. Pia tunatoa masomo katika
shahada ya kwanza, shahada ya pili na shahada ya tatu.
Josefu: Asante sana kwa msaada wako. Kwaheri.
Mwenyeji: Karibu tena.