Wanafunzi wakimaliza shule za upili (sekondari) wanaweza kwenda
kusoma katika shule za ufundi. Katika shule za ufundi wanafunzi
hufundishwa ufundi chuma, uchongaji, uhandisi umeme, na uhandisi
chuma.
Juma na Asha ni majirani. Juma ni mwanafunzi. Yeye anasoma katika
shule ya ufundi. Asha ni mfanya biashara.
Asha: Hujambo Juma?
Juma: Sijambo. Habari za biashara?
Asha: Nzuri. Habari za shule?
Juma: Salama tu.
Asha: Juma, ninyi mnajifunza nini katika shule ya ufundi?
Juma: Tunajifunza fani mbalimbali kama useremala, ufundi chuma,
kuchonga fanicha
mbalimbali kama vitanda, viti,
meza,
makabati, n.k.
Asha: Je, wanafunzi wakimaliza shule wanafanya nini?
Juma: Wanafunzi wakimaliza shule wanaweza kuajiriwa na serikali au mashirika mbalimbali. Pia
wanaweza kuanzisha miradi yao binafsi.