|
VIJIJI
Asilimia kubwa
ya wananchi wengi wa Tanzania wanaishi vijijini. Katika Tanzania, kuna vijiji
vya aina mbalimbali, vikubwa na vidogo. Wananchi wengi wa vijijini wanajishughulisha na
shughuli za ukulima na ufugaji.
Vijijini, mara nyingi watu hutembea
kwa miguu, na hubeba
mizigo yao vichwani. Vijiji vingi vimezungukwa na
mazingira mazuri ya kupendeza machoni. Watu wengi wa vijijini hutumia kuni kwa mapishi.
Mara nyingi, akina mama huenda msituni kutafuta kuni.
Watoto wa vijijini huwasaidia wazazi wao katika shughuli mbalimbali kama kubeba
mizigo, kuchota
maji, na hata kuangalia mifugo.
Majengo ya
nyumba za vijijini ni tofauti sana na yale ya mijini. Nyumba nyingi za vijijini
hujengwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo.
Mara nyingi nyumba hizi huezekwa kwa makuti na
mara nyingine huezekwa kwa mabati.
Katika vijiji, wanavijiji huwa na maeneo makubwa
ambayo pia huyatumia katika shughuli za ukulima na ufugaji.
|