|
KISIWA CHA ZANZIBAR
Historia ya Tanzania ni historia ya wakoloni mbalimbali, waarabu, Wajerumani, na Waingereza. Historia hii inaonekana wazi katika majumba na magofu yaliyopo sehemu za pwani hasa Unguja na Bagamoyo. Kwanza tutatembelea mji wa Unguja kuona mambo yanayotukumbusha historia hizo.
Majengo haya ya kizamani mjini
Unguja yanatukumbusha kwamba Unguja ilitawaliwa na
Waarabu. Ujenzi wa majumba haya unafanana sana
na ujenzi wa majengo huko Uarabuni.
Magofu haya yanajulikana kama magofu ya Maruhubi. Maruhubi ni jina la aliyekuwa
mwenye shamba mahali hapa. Baraghas ni mfalme wa
tatu katika wafalme waarabu waliotawala Zanzibar. Alijenga hapa kasri yake.
Kasri ilikuwa ya kuweka masuria wa
mfalme Baraghash.
Idadi ya vyumba vilivyomo, pengine ni
sawa na idadi ya masuria waliokaa hapa. Mwaka 1899, ajali ya moto iliiteketeza. Hamam ambayo
ujenzi wake unafanana sana na mahamam ya kituruki, ilinusurika.
|