Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 8: Sehemu za pwani > Lesson 4:

    

MJI WA GEDE 

Magofu ya Gede ni mabaki ya majengo ya zamani ambayo yamebaki baada ya utawala Mazrui. Mabaki ya haya ni majumba, misikiti, na nyumba za mashekhe wa kimazurui. Majumba haya yana historia ya ukoloni wa nchi ya Kenya. Mabaki ya majumba haya ya zamani yanaonyesha jinsi ujenzi wa karne hizo ulivyokuwa madhubuti. Kwa sababu kuta hizi ni nene sana, mabaki yake bado yanaonekana hata baada ya miaka mingi kupita. Tunaona pia mabaki ya msikiti wa zamani. Ukoo wote wa Mazrui ulikuwa ni waisilamu na walikuwa na misikiti yao binafsi. Kibla cha msikiti huu bado kimebaki imara. Baadhi ya wafalme waliokuja kutawala Gede walikaa katika nyumba hizi pia.

© African Studies Institute, University of Georgia.