MJI WA MOMBASA
Sasa tunatembelea mji wa Mombasa. Kutokana na historia yake, mji wa Mombasa
umegawanyika katika sehemu mbili: mji wa zamani na mji wa kisasa.
Mji wa zamani uliejengwa katika enzi za
waarabu. Kwa hivyo, majengo yake yana nakshi zinazofanana sana
na nakshi za Bara
Arabu. Mji wa kisasa una majengo ya kisasa yanayofanana
sana na majengo ya Ulaya.
Historia ya mji wa Mombasa ni historia ya vita mbalimbali, baina ya wenyeji, Waarabu, Wareno na Waingereza. Historia hii imehifadhiwa katika jumba la makumbusho katika ngome ijulikanayo kama Fort Jesus.
Kama
tunavyoona, ngome hii ni kubwa sana. Ilikuwa makao
makuu ya ulinzi,
pia mahifadhi ya zana zote za vita. Pia mahabusu waliotekwa katika vita waliwekwa
hapa. Kabla ya vita, ngome hii ilikuwa soko kubwa la watumwa waliopelekwa Bara
Arabu na sehemu nyingine duniani. Mizinga katika
ngome hii ni ile iliyotumiwa katika vita mbalimbali hapa mjini Mombasa. Kudumu kwa
ngome hii kunatokana na kufanyiwa marekebisho kila
baada ya muda
fulani. Hii ni muhimu ili kuhifadhi kikamilifu mambo
ya historia ya Kenya
|