Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 8: Miji > Lesson 6:

    

MJI WA DAR ES SALAAM 

Sasa tuko mjini Dar-es-Salaam. Mji wa Dar-es-Salaam ni mkubwa sana. Kuna majumba mengi ya kizamani na ya kisasa. Shughuli mbalimbali hufanywa kando kando ya barabara hizi.

Hapa tunaona biashara za bidhaa ndogo ndogo kama vile vitabu, magazeti, vifaa vya shule kama kalamu, bahasha na kadhalika. Wauzaji hujipatia pato dogo kwa kuendeleza maisha yao.

Hili ni jumba la sinema. Tunaona watu wako nje tayari kununua tikiti za kuingia ndani ili kujipumbaza kwa kuangalia picha. Hapa tunaona barabara, majumba mazuri, na maduka ya kuuza bidhaa na vifaa mbalimbali. Hii ni mitaa tofauti ya mjini Dar-es-Salaam. Huu ni mtaa wa Samora. Dereva wa motokaa hizi wanajua kwamba ni lazima kuendesha motokaa zao upande wa kushoto kama Uingereza na sio upande wa kulla kama Amerika na Ufaransa.

Hii ni hoteli ya Kilimanjaro. Hoteli maarufu mjini Dar-es-Salaam, na mojawapo ya hoteli za watalii. Vyakula mbalimbali vya asili hupikwa na kuuzwa hapa. Wageni wengi wanapenda kujaribu mapishi haya ya kitamaduni. Kama tunavyoona hapa, kuna wageni na wenyeji pia ambao wanakula chakula cha mchana hapa. Baadhi ya vinywaji hapa kama vile konyagi, hutengenezwa katika viwanda vya Tanzania.

© African Studies Institute, University of Georgia.