KIWANJA
CHA NDEGE CHA DAR ES SALAAM
Wageni wengi wanapokuja Tanzania wanasafiri kwa ndege au eropleni. Kuna viwanja viwili vya kimataifa Tanzania. Kiwanja cha kimataifa cha Kilimanjaro ambacho kiko Arusha, na kiwanja cha kimataifa cha Dar-es-Salaam ambacho kiko Dar-es-Salaam.
Leo tutatembelea kiwanja cha Dar-es-Salaam. Kiwanja hiki kinapokea ndege za kimataifa za Uingereza, Uholanzi, Uswisi, Ufaransa, Bara Arabu, Zimbabwe, Kenya na kadhalika.
Kuna taratibu mbalimbali wakati wageni wanapofika nchi yoyote. Kuna ukaguzi wa afya, ukaguzi wa pasi au pasipoti na ukaguzi wa mizigo. Tumfuate msafiri mmoja jina lake Clemence. Tangu anapoingia mpaka anapotoka katika jengo la abiria wa ndege ya KLM.
|