Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 9: Usafiri wa Anga > Lesson 2:

    

MSAFIRI CLEMENCE

Clemence: Habari za hapa?

Afisa Afya: Salama. Habari za safari?

Clemence: Safi.

Afisa Afya: Eee, habari za huko?

Clemence: Salama, salama.

Afisa Afya: Ndiyo, ndiyo.

Clemence: Hamjambo hapa?

Afisa Afya: Aah. Hatujambo. Karibu sana.

Clemence: Asante.

Sasa tumfuate msafiri Clemence tena, na tusikilize
mazungumzo yake na maafisa wa afya, uhamiaji, na ushuru.
Afisa Afya: Umetokea wapi?

Clemence: Nimetokea Georgia.

Afisa Afya: Umetokea Georgia?

Clemence: Marekani.

Afisa Afya: Aha, katika siku kumi zilizopita kabla ya kuanza safari yako, uliwahi kwenda sehemu nyingine yoyote?

Clemence: Ndiyo. Tulikuwa Texas, tukaja New York, halafu nimepitia Amsterdam na nimefika hapa.

Afisa Afya: Ndiyo. Unayo kadi yako ya kuchanja?

Clemence: Nimekupa. Hiyo hapo.

Afisa Afya: Asante.

© African Studies Institute, University of Georgia