Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 9: Usafiri wa Barabara > Lesson 3:

    

VYOMBO VYA USAFIFI WA BARABARA

Wananchi wa sehemu mbalimbali za Tanzania wanategemea sana usafiri wa barabara. Watu wengi hutumia usafiri huu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Usafiri wa barabara ni mashuhuri na ni usafiri wa kuaminika sana. Serikali na wananchi hutumia usafiri wa barabara kwa kusafirishia vitu mbalimbali kama bidhaa, mazao, mifugo na kadhalika. Usafiri wa barabara hutumia vyombo mbalimbali kama magari madogo na makubwa, malori, mabasi, pikipiki na baisikeli.

Katika sehemu za mashambani, matrekta hutumiwa kama mojawapo ya vyombo vya usafiri. Katika miji mikubwa kama Dar-es-Salaam, wananchi wengi hawana magari binafsi. Hivyo, hutumia mabasi kwenda makazini, maofisini, na katika shughuli mbalimbali. Pia siku hizi, kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri wa barabara, aina mbalimbali za magari hutumiwa katika kusafirisha abiria.Katika nchi ya Tanzania, magari hupita upande wa kushoto wa barabara. Hii ni kutokana na historia yake ya kutawaliwa na Uingereza. Hivyo, sheria nyingi za usalama barabarani zinafanana sana na zile za nchi ya Uingereza.

© African Studies Institute, University of Georgia