|
KUTEMBEA
KWA MIGUU
Katika
sehemu nyingi za Tanzania, watu wengi hutembea kwa miguu kwenda
sehemu mbalimbali. Kuna sababu mbalimbali zinazofanya watu wengi
watembee kwa miguu. Moja,
watu wengi hawana magari binafsi, hivyo, hutembea kwa miguu au hutumia magari
ya abiria. Pili, watu wengi hufanya shughuli zao nyingi katika maeneo ya
karibu karibu, hivyo, hakuna haja ya kutumia mabasi au mabasi. Kwa mfano,
katika mitaa mingi
ya Dar-es-Salaam kuna maduka ya bidhaa mbalimbali, hivyo watu huenda madukani
kwa miguu kwa sababu maduka hayo huwa yapo karibu sana na sehemu wanazoishi.
Kwa kawaida watu wengi hutembea kwenda makazini, maofisini, madukani, sokoni, na hata kuwatembelea ndugu na marafiki wanaoishi sehemu za jirani. Pia, wanafunzi wengi hutembea kwenda mashuleni.
Pia mara nyingi watu wanaotembea kwa miguu huwa wanabeba mizigo yao
mikononi au vichwani. Njia ya ubebaji mizigo Kichwani ni maarufu sana katika
sehemu nyingi za Afrika. Watu wengine huweza kubeba mzigo yenye uzito wa
zaidi ya kilo ishirini. Pia watu wengine huweza kufanya kazi ya uchukuzi wa
mizigo midogo midogo kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine. Watu hawa hubeba
vitu mbalimbali kama matunda, au majani ya kulisha ngombe.
|