|
WAKULIMA WADOGO WADOGO
Uchumi wa sehemu nyingi za Afrika, hasa Afrika ya mashariki unategemea wakulima wadogo wadogo. Asilimia tisini na tano ya wakulima hawa ni wanawake na wanakaa vijijini. Mashambani kuna mazao mbalimbali ya chakula na biashara. Kwanza tutatembelea mashamba Zanzibar. Kuna mashamba ya watu binafsi na mashamba ya serikali. Katika mashamba ya serikali na mashamba ya watu binafsi, tunaweza kuona mikarafuu, miti ya iliki, mihindi, mchicha, migomba ya ndizi, hasa gonja na kisukari,pilipili manga, mihogo, minazi, mdalasini, mashamba ya mpunga, michungwa, mtama, minanasi, mawese, kungumanga, ndimu, maembe na mikorosho.
|