Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 11: Ukulima > Lesson 2:

    

KUTEMBELEA MKULIMA

Sasa tutakwenda shambani. Tutaongozana na bwana shamba. Jina la bwana shamba ni Hasani Kilima. Atatupeleka kumuona mkulima shambani. Jina la mkulima ni Ramadhani Kasi. Yeye analima mpunga na maharagwe. Lakini sasa anaanza kuotesha maharagwe kwa sababu amemaliza kuvuna mpunga.

Mkulima: Huwa tunatumia kupanda kwa kutumia kamba na vipimo vya futi tatu, halafu na mbolea ya kukuzia. Eee.

Msaili: Ushauri huo mmeupata wapi?

Mkulima: Huwa tunajaribu kupata kwa mabwana shamba. Wanatujulisha.

Msaili: Wanawatembelea hapa, au mnawatafuta?

Mkulima: Ata, huwa wanatutembelea. Tatizo ni kwamba, huwa tunasumbuliwa na nyasi. Eeh, nyasi ambalo linakuwa jingi sana; ni kiasi ambacho tunashindwa hata jinsi ya upaliliaji. Tunaomba tupate ile dawa ya kuuwa magugu.

Msaili: Kwa hiyo shida kubwa ni ipi? Magugu?

Mkulima: Ndiyo, ndiyo.

Msaili: Tuone eneo lako unalolima na pia kupata maelezo yako kuhusu shughuli za kilimo unavyofanya ili wageni waone hapa. Pia waweze kwenda kuwaonyesha wenzao, watanzania wanafanya shughuli gani.

Mkulima: Ndiyo, ndiyo. Sawa.

Msaili: Tunashukuru sana.

Mkulima: Asante

© African Studies Institute, University of Georgia.