Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 11: Ufugaji > Lesson 3:

    

UFUGAJI WA WANYAMA

Hapa ni mradi wa mbuzi wa maziwa. Mbuzi hawa wamejengewa vibanda ghorofani ili kuzuwia magonjwa.

Hapa ni banda la mbuzi. Hawa tunawalisha kwa ndani. Kwa hiyo, majani, pumba na chakula chote wanapata ndani ili kuweza kuzuwia magonjwa. Na tumejenga mjengo huu wa ghorofa kwa ajili ya kuzuwia magonjwa. Na kuna mbuzi sita ambao mmoja ni dume na yaliyobakia watano ni majike. Ni aina ya kisasa ambao wanatoa maziwa.

Hapa ni mradi wa ngombe wa maziwa. Wanafunzi wanafundishwa juu ya utunzaji bora wa mifugo na magonjwa yake. Ujuzi huu wataupeleka vijijini; watajaribu kuutumia na kuwafundisha wengine. Ngombe mmoja anaweza kutoa maziwa ya kutosha kwa familia nzima.

Huu ni mradi wa nguruwe. Mradi huu unapendwa sana na wanavijiji kwa sababu nguruwe huzaana mapema.

© African Studies Institute, University of Georgia.