Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 11: Ufugaji > Lesson 4:

    

MRADI WA KUKU

Baada ya kutoa maagizo, mama Mwisongo anatembelea sehemu mbalimbali za miradi yao. Kwa sababu ya ukubwa wa miradi hii, kuna wafanyakazi wa kuwasaidia. Miradi ni mradi wa kuku wa nyama, mradi wa kuku wa mayai, mradi wa ngombe, mradi wa kutotoa vifaranga.

Wafanyakazi wanasafisha mabanda ya kuku. Wanawapa kuku chakula. Wanasafisha vyombo vya chakula cha kuku. Wanawalisha ngombe. Wanakusanya mayai katika mabanda. Wanachagua mayai ya kuuza. Wanachagua mayai ya kutotolea vifaranga, na wanawakamua ngombe kupata maziwa.

© African Studies Institute, University of Georgia.