Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 11: Uchongaji na useremala > Lesson 5:

    

UCHONGAJI

Sanaa ni utamaduni na utamaduni ni sanaa. Kwa waafrika, na watanzania kwa ujumla, sanaa ni sehemu muhimu ya historia na utamaduni. Kwa watanzania wengi, sanaa ni kipaji; sio jambo linalofundishwa mashuleni.

Hiki kinaitwa kijiji cha wachongaji. Wasanii mbalimbali wamejiunga kufanya ushirika. Kwa pamoja wanachonga vinyago mbalimbali. Vinyago hivi huuzwa rejareja kwa watu binafsi, hasa watalii. Vinyago vingi huuzwa kwa ujumla kwa wafanyabiashara wa Ulaya, Amerika na Asia.

Kinyago hiki kinaitwa ujamaa. Wachongaji wanatumia patasi, visu na msasa katika kazi hii ya uchongaji. Kuchonga si kazi rahisi. Hutegemeana na ukubwa wa kinyago. Uchongaji wake unaweza kuchukua kati ya siku moja hadi miezi mitatu.

Je, wachongaji wanaweza kujipatia mtaji wao kwa kazi hii ya uchongaji?

Ndiyo, kwa sababu hufanya kazi pamoja kwa ushirika wao. Chama chao cha ushirika kinawapa ruzuku ya wiki, na baada ya kuuza vinyago wanagawana pesa.

© African Studies Institute, University of Georgia.