|
USEREMALA
Wanafunzi
ambao wanamaliza shule za upili, yaani shule za sekondari wanaweza
kwenda kusoma katika shule za serikali za ufundi. Sasa tutatembelea shule ya
sekondari ya ufundi huko kisiwani Unguja. Wanafunzi katika shule hizi hufundishwa
ufundi wa chuma, uchongaji, uhandisi
umeme na uhandisi chuma. Baada ya kumaliza masomo yao, wanaweza kuajiriwa na
serikali kufanya kazi katika mabohari ya
serikali, au kampuni za watu binafsi. Wengine wanaanzisha miradi yao binafsi.
Kwa mfano, vijana hawa katika mitaa ya
Unguja. Hawa vijana wa Unguja wanatengeneza fanicha za nyumbani kama vile vitanda, meza na viti.
Pia wanachonga milango na madirisha ya nakshi,
na pia mitumbwi.
Vijana wa Morogoro wanatengeneza vifaa vya bati kama vile ndoo za
maji, ndoo za kumwagilia mimea maji katika bustani, vibatari, taa na
vyombo vya kulishia kuku.
|