Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 13: Desturi za Arusi > Lesson 1: Hide transcript

    

SHEREHE YA BWANA ARUSI: WAISLAMU

Bwana arusi anavaa kanzu na kofia. Bibi arusi anavaa gauni refu na anajitanda leso kubwa au ushungi kichwani. Sherehe za arusi ziko za aina tatu: sherehe ya arusi, sherehe ya bwana arusi, na sherehe ya bibi arusi. Katika sherehe ya bwana arusi, wanaume tu wanahudhuria. Sherehe ya bibi arusi, wanawake tu wanahudhuria. Sherehe hizi hufanywa baada ya sherehe ya arusi, yaani baada ya kufunga ndoa msikitini. Hatutaona sherehe ya msikitini bali sherehe ya wanaume na sherehe ya wanawake.

Hapa tunatazama sherehe ya wanaume. Wanaingia katika ukumbi wa karamu, wanakaa juu ya mikeka na wanamsubiri bwana arusi. Sasa bwana arusi anaingia na anakaa katika sehemu yake maalumu.

Sasa vyakula vya karamu vinaandaliwa. Chakula ni biriani. Wanakula kwa mikono kufuatana na desturi zao.

 

© African Studies Institute, University of Georgia.