Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 13: Sherehe ya Binti Arusi > Lesson 2: Hide transcript

    

SHEREHE YA BIBI ARUSI: WAISLAMU

Ama kweli binti sasa ni mrembo, tayari kwa sherehe za arusi. Wanawake wa pande zote mbili hujipamba kama bibi arusi. Tutawaona pia katika sherehe ya bibi arusi.

Sasa tunatazama sherehe ya bibi arusi. Sherehe hufanywa nyumbani kwa wazazi wa bi-arusi. Ndugu na marafiki wa upande wa bwana arusi hualikwa pia. Sherehe huanza kwa nyimbo, ngoma na vigelegele.

Sherehe ya bibi arusi wanawake tu wanahudhuria. Sherehe hizi hufanyawa baada ya sherehe ya arusi. Yaani baada ya kufunga ndoa msikitini. Hatutaona sherehe ya msikitini bali sherehe ya wanaume na sherehe ya wanawake.

 

African Languages Program, University of Georgia