Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 13: Desturi za Arusi > Lesson 5: Hide transcript

    

Bwana Arusi anafika kanisani

Hili ni gari lililomleta bwana arusi. Bwana arusi amevaa mavazi ya kisasa. Pamoja naye ni binti wa maua na kijana atakayebeba pete za arusi. Hii ni desturi ya kigeni.

Hawa ni wanawake kutoka katika familia ya bwana arusi. Jamaa ya bwana arusi bado inamsubiri bibi arusi ambaye amechelewa sana. Ili kupitisha wakati, wanawake wanaimba na kucheza ngoma za kijadi chao. Wanawake wamevalia sare, gauni au kanga. Hii ni desturi ambayo makabila mengi hufuata siku hizi.

 

African Languages Program, University of Georgia