Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 13: Bibi Arusi anafika Kanisani > Lesson 6: Hide transcript

    

BIBI ARUSI ANFIKA KANISANI

Mwishowe bibi arusi na familia yake wanafika baada ya saa nzima. Kwa kuwa wamechelewa sana, wanawake wa familia ya bwana arusi wanaimba: "Umetuchelewesha".

Kwa kujaribu kueleza kwa nini wamechelewa, wanawake wa upande wa bibi arusi wanajibu kwa wimbo: "Anameremeta". Yaani walichelewa kwa sababu walikuwa wanampamba bibi arusi na sasa anameremeta kama nyota.

 

African Languages Program, University of Georgia