SIKU
YA I JUMAA
Tanzania ni nchi yenye uhuru wa dini. Kwa hivyo, wananchi ambao ni Waislamu wana uhuru wa kufuata kanuni na masharti ya dini ya kiislamu bila kuogopa. Kadhalika, Wakristu wana uhuru wa kufuata kanuni na masharti ya dini ya kikristu bila kuogopa.
Kwa Waislamu, sala ya Ijumaa ni sharti mojawapo. Kwa hivyo, serikali inawaruhusu
wananchi wote Waislamu kuondoka kazini mapema au kuacha shughuli zote
ili kwenda msikitini kusali. Kwa kawaida sala ya Ijumaa inaweza
kuanza kati
ya saa sita mchana na saa saba mchana.
|