Sala ya Ijumaa
Huu ni msikiti. Sasa waislamu wanaingia msikitini kusali sala ya Ijumaa. Kwanza
Khatibu hutoa hotuba. Yeye husimama katika mimbari na hushika fimbo. Fimbo
hii ni
alama ya uongozi. Kwa kawaida Khatibu huvaa kanzu, juba, kofia na kashda. Baada
ya hotuba watu husali sala ya Ijumaa. Sala huongozwa na Imamu. Kwa kawaida
watu huvaa nguo mbali mbali kama kanzu, koti, juba, kashda na kofia.
Mwenye
enzi Mungu mkubwa
Mwenye enzi Mungu mkubwa
Nashuhudia hakuna anayeabudiwa kwa haki ila mwenye enzi Mungu
Nashuhudia hakuna anayeabudiwa kwa haki ila mwenye enzi Mungu
Nashuhudia kwamba Mohamed ni mjumbe wa mwenye enzi Mungu
Nashuhudia kwamba Mohamed ni mjumbe wa mwenye enzi Mungu
Njooni msali
|