Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 16: Dini > Lesson 3: Hide transcript

    

SIKU YA JUMAPILI

Kwa wakristu, siku ya sala, kwa kawaida, ni Jumapili. Siku hiyo ni siku ya mapumziko kwa wananchi wote. Kwa hivyo si lazima serikali iwaruhusu wakristu kuacha shughuli zao na kwenda kanisani.

Kwa wakristu wengi, Jumapili ni siku ya kwenda kanisani wa sababu wengi hawana nafasi kwenda kanisani kila siku. Ni siku ya kumshukuru Mungu kwa wiki ya kazi, afya, na mambo yote mazuri ambayo yamewatokea.

Kwenda kanisani pia ni njia mojawapo ya watu kukutana na marafiki na jamaa. Kabla na baada ya sala, watu huamkiana na huzungumza.

 

© African Studies Institute, University of Georgia