SIKUKUU
YA KIPAIMARA
Ingawaje
picha hizi ni za sala ya Jumapili, hii si Jumapili ya kawaida.
Ni jumapili maalum. Ni siku ya Kipaimara. Siku ya Kipaimara ni
siku ambayo watoto wenye umri wa miaka kumi na zaidi wanapokelewa
rasmi katika kanisa kama wakristu kamili. Siku hiyo askofu ambaye
ni mkuu wa kanisa, anafika na kuendesha sala. Huyu ni askofu na
wasaidizi katika sherehe hii ya Kipaimara. Kwa sababu ni sherehe
maalum, washiriki wamevalia mavazi rasmi sana. Kwa sababu ni sherehe
ya Kipaimara washiriki wanaingia kanisani katika mistari na kukaa
katika sehemu maalum.
Kwaya ya kanisa imejiandaa. Nyimbo zao ni maalum kwa sherehe ya leo. Sasa
askofu anawapa watoto washiriki sakramenti ya Kipaimara. Kila mshiriki
anaongozwa na mdhamini wake. Kwa mfano huyu ni mshiriki. Huyu ni mdhamini
wake. Sasa
washiriki wanachukua zawadi zao na kuzipeleka mbele ya Askofu ambaye
atazipokea kwa niaba ya kanisa.
|