Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 16: Dini > Lesson 5: Hide transcript

    

HISTORIA YA KANISA LA KIANGLIKANI

Sehemu nyingine ya historia hapa Zanzibar ni kanisa la Kianglikani ambalo limejengwa mwaka 1873. Umaarufu wake unatokana na historia inayomhusu Askofu Steer. Kanisa hili linatembelewa sana na wageni wanaokuja Zanzibar. Ni bora tuingie ndani na tumsikilize kiongozi wa wageni. Yeye atatutolea historia fupi ya kanisa hili na habari za Askofu Steer.

Hili ni kanisa la Kianglikana la Zanzibar Kathedro. Kanisa hili kabla ya kujengwa lilikuwa soko la watumwa. Na lilijengwa mwaka 1873 na bishop Edward Steer ambaye ndiye aliyekabidhiwa kazi hiyo. Hapa Zanzibar utumwa ulikomeshwa mwaka 1873 Askofu. Na sehemu hii aliuziwa mhindi mmoja ambaye anaitwa Jeram Sandhi. Alinunua sehemu hii na kumkabidhi bishop Edward Steer ili kulijenga kanisa. Kanisa hili lilifunguliwa mwaka 1873. Hapo ndipo ilikuwa ni siku yake ya mwanzo kufunguliwa na lilifunguliwa likiwa halina paa. Lilisherehekewa kama ufunguzi wake rasmi hapa Zanzibar, mwaka huo huo wa 1873.

Dirisha hilo hapo la pili ni ukumbusho wa Dr. Livingstone na wafumbuzi wengine ambao walifika kutembelea sehemu za Afrika ya Mashariki mnamo karne ya 19. Na baadaye kwenda Uingereza ili kutoa maelezo kuhusu biashara hii ya utumwa. Ndipo alipochaguliwa Bishop Edward Steer kuja Zanzibar ili kujenga hili kanisa na ambapo sasa watu ndio wanaendelea kusalia na bado linatumika kwa kusaliwa.

 

© African Studies Institute, University of Georgia