Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 16: Fill-in > Lesson 6: Hide transcript

    

MSIKITI WA ZAMANI WA BAGAMOYO

Halafu hao wapersia walikuwa waislamu. Sasa madhehebu ya kiislamu ni lazima watawadhe kabla ya kusali. Hivyo wanachukua maji haya wanaweka nyuma ya ukuta huo panaitwa hodhi wanaosha uso na mikono. Baadaye wanajaza hapa tena. Hii inaitwa birika. Wanaosha miguu hapa. Halafu hao waliokwishaosha mmoja wao anapanda juu ya ngazi hizo. Anapanda hapa mpaka juu. Anaangalia usawa wa Makka. Anaadhini kuita watu kuja kusali. Ni mara tano kwa siku moja kwa madhehebu yao ya Kiislamu. Na kabla ya hivyo sehemu yote hii ilikuwa imefukiwa chini ya ardhi. Tumefanya kupafukua mwaka elfu moja mia tisa na hamsini na nane na mwingereza mmoja anayeitwa Neville Chittick. Hivyo kuna kibao cha mti hiki hapa tumeikweka kuzingia huu ukuta pamoja na hiki chuma kusaidia kwa sababu palikuwa pamekatika.

Sasa tuone ndani ya msikiti. Hayo mapande mapande ni dari la huo msikiti. Lilikuwa limeshikiliwa na miti migumu sana mikoko alama zake ni hizi na kuna tundu kwenye kuta lakini walipataje simenti (saruji) na karne ya kumi na tatu simenti (saruji) ilikuwa haijagunduliwa? Ujuzi waliokuwa wakiutumia ni kuchoma haya matumbawe ambapo yanakaa baharini wakija wakiyachukua kule baharini wakija hapa nchi kavu wanapanga kuni na wanayachoma haya mawe. Wakiyachoma wanapata chokaa. Baadaye chokaa yake wanachanganya na michanga yetu hii wanachimba shimo kubwa wanazika na wanasubiri kwa miaka mitatu. Baadaye wakichimbua hiyo sehemu wakivuruga tena kwa maji inatokea aina ya sumu yenye mnato kwa lugha ya kigeni inaitwa carbon dioxide. Kwa hivyo idadi ya tope zote zinanata ndiyo tunapata simenti (saruji) ya chokaa. Halafu na huku juu wanasiriba siriba juu yake kabisa kwa sababu mabati karne ya kumi na tatu yalikuwa hayajagunduliwa.

Sasa kama hilo dari limebomoka lakini kibla yake bado iko nzima. Kibla hiyo ya karne ya kumi na tatu. Kibla ni sehemu anaposimama kiongozi wa sala kwa wakati ule anayeitwa imamu. Ni lazima aende hapa na kusema Allah Akbar. Samia llaahu liman hamida. Na wengine nyuma wanasimama wote wakimfuata yeye anavyofanya bali tu wote ni lazima waangalie usawa wa Makka. Pia inambidi huyu imamu atumie sauti kubwa kwa sababu katika madhehebu ya waislamu wanawake wanakaa sehemu yao na wanaume sehemu yao. Kwa hivyo sehemu hii moja, mbili, tatu hapa ni wanaume na kule ni wanawake. Mnaweza kuja kuona.

© African Studies Institute, University of Georgia