Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 2: Kujua Nambari > Lesson 4: Miezi

    

MIEZI YAMWAKA. MONTHS OF THE YEAR

Gilbert: Hodi.

Sakina: Karibu.

Gilbert: Habari za hapa?

Sakina: Nzuri tu. Karibu ukae.

Gilbert: Asante. Nimekuja kuwaaga.

Sakina: Utarudi lini kutoka Tanzania?

Gilbert: Mwezi wa nane tarehe 20. Nitaendelea kuandika tasnifu yangu kutoka mwezi wa tisa mpaka mwezi wa kumi na mbili

Sakina: Utafanya nini baada ya kumaliza masomo yako?

Gilbert: Nitarudi Tanzania. Nitaanza kufundisha katika chuo kikuu cha Dar-es-Salaam mwezi wa pili au mwezi wa tatu.

Sakina: Safari njema na bahati njema katika kuandika tasnifu yako.

Gilbert: Asante. Haya kwaheri.

Sakina: Kwaheri ya kuonana.

Gilbert: Haya.

 

 

 

© African Studies Institute, University of Georgia.