Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 2: Kujua Nambari > Lesson 6: Mwaka wa ngapi

    

MWAKA WA NGAPI? (WHAT YEAR?)

Naima: Amini, watoto wako wanasoma wapi?

Amini: Helena anasoma chuo kikuu cha Dar-es-Salaam. Yeye anasoma mwaka wa tatu. Yeye atamaliza shule mwezi wa sita mwakani. Batuli anasoma chuo kikuu cha Sokoine. Yeye anasoma mwaka wa pili. Na John anasoma chuo kikuu cha Dar-es-Salaam. Yeye anasoma mwaka wa kwanza. Wote wanataka kuwa walimu wakimaliza masomo yao.

Naima: Hongera. Mimi pia, watoto wangu wanasoma chuo kikuu cha Dar-es-Salaam. Amina anasoma mwaka wa pili na Ali anasoma mwaka wa nne. Amina anataka kuwa daktari na Ali anataka kuwa mhandisi.

Amini: Vizuri sana.

 

 

 

© African Studies Institute, University of Georgia.