Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 4: Wakati. Telling the time > Lesson 1: Kesho utafanya nini?

    

KESHO UTAFANYA NINI? WHAT WILL YOU DO TOMORROW?

Amini: Hujambo Anita?

Anita: Sijambo. Habari za asubuhi?

Amini: Nzuri. Habari za nyumbani?

Anita: Salama tu.

Amini: Utafanya nini kesho?

Anita: Kesho. Kesho nitafanya shughuli nyingi. Asubuhi nitafanya usafi wa nyumba yangu. Mchana nitakwenda mkutanoni mpaka alasiri. Na jioni nitakwenda nyumbani kwa mama mdogo

Amini: Mimi nitafanya shughuli nyingi pia. Asubuhi nitakwenda hospitali. Mchana nitakwenda madukani. Na magharibi nitapumzika nyumbani.

Anita: Sasa unakwenda wapi?

Amini: Sasa ninakwenda nyumbani.

Anita: Haya kwaheri.

Amini: Kwaheri ya kuonana.

 

© African Studies Institute, University of Georgia.