Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 4: Wakati. Telling the time. > Lesson 4: Wakati wa shughuli mbali mbali

    

WATAKATI WA SHUGHULI. (TIME OF ACTIVITIES)

Josefina na Gilbert ni marafiki. Wao wanazungumza juu ya ratiba zao.

Gilbert: Hujambo Josefina?

Josefina: Sijambo. Habari za leo?

Gilbert: Nzuri tu. Habari za nyumbani?

Josefina: Salama.

Gilbert: Kesho utafanya nini?

Josefina: Kesho. Kesho nitafanya shughuli nyingi. Saa moja asubuhi nitakwenda kazini. Saa tano asubuhi nitakwenda hospitali. Saa nane mchana nitasafisha nyumba. Saa kumi na mbili jioni nitakwenda kanisani. Saa nne usiku nitakwenda kulala.

Gilbert: Mimi pia nitakuwa na shughuli nyingi. Saa asubuhi moja nitakwenda kazini. Saa tisa mchana nitarudi nyumbani. Saa kumi na moja alasiri nitakwenda mpirani, na saa mbili usiku nitakwenda mkutanoni.

Josefina: Haya tutaonana baadaye.

Gilbert: Haya. Baadaye.

 

© African Studies Institute, University of Georgia.