Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 7: Shule za Watoto > Lesson 2:

    

MAZUNGUMZO NA MWALIMU 

Msaili: Mwalimu, hii shule inachukua wanafunzi wa aina gani?

Mwalimu: Tunachukua wanafunzi kuanzia miaka minne hadi sita. Tunafundisha miaka mitatu hapa. Mwaka wa kwanza, wana umri wa miaka minne. Mwaka wa pili na mwaka wa tatu wanasoma pamoja. Hawa ni wanafunzi wa mwaka wa pili na mwaka wa tatu. Wote wana miaka sita. Mwakani wataingia shule ya msingi darasa la kwanza.

Msaili: Kuna walimu wangapi?

Mwalimu: Kuna walimu kumi na mbili. Kila darasa walimu wawili wawili. Asubuhi kuna madarasa mawili ya wanafunzi wa mwaka wa pili na mwaka wa tatu. Yaani wanafunzi wa miaka sita. Mchana ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Wana miaka minne. Wanafunzi wote wanavaa sare. Wasichana, gauni la buluu na blauzi nyeupe. Wavulana, shati jeupe na kaptula ya buluu.

Msaili: Asante sana.

© African Studies Institute, University of Georgia.