Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 7: Shule za Dini > Lesson 3:

    

SHULE YA KIISLAMU 

Sasa tunatembelea madarasa katika shule ya kiislamu ya Bakathir mjini Zanzibar. Misingi ya madrasa ni uislamu. Shughuli zote za mafunzo zinazingatia msimamo wa dini ya kiislamu.

Walimu wote wa madrasa ni wanaume; tofauti na shule za watoto wadogo. Walimu wote katika shule za watoto wadogo ni wanawake. Kama shule za watoto wadogo, madrasa yanaanza na mkutano wa sala. Mkutano unaongozwa na mwalimu mkuu wa madrasa.

Ni wazi kwamba masuala ya jinsia ni muhimu katika utamaduni wa dini ya kiislamu. Hapa tunaona wazi msisitizo wa tofauti za kijinsia. Nafasi ya wanawake ni tofauti na nafasi ya wanaume katika dini na katika jamii.

© African Studies Institute, University of Georgia.