Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 7: Shule za Dini > Lesson 4:

    

CHUO CHA ASKOFU KISANGI 

Kituo cha Askofu Kisanji kina sehemu ya watoto pia. Lengo la kituo cha watoto ni kuwapa wanafunzi ujuzi wa kufundisha; pia ujuzi wa kuendesha vituo vya watoto wadogo katika miji au vijiji vyao.

Baadhi ya watoto katika shule hii ni watoto wa wanafunzi katika chuo cha Askofu Kisanji. Wengine wanatoka katika vijiji vya karibu na shule. Sasa tuwatembelee watoto hawa pamoja na walimu wao.

Watoto hawa wanajiandaa kwa masomo ya darasa la kwanza katika shule za misingi. Kwa sasa wanafundishwa kusoma, kuhesabu, dini na kuandika.

© African Studies Institute, University of Georgia.