Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 7: Elimu ya juu > Lesson 6:

    

CHUO CHA UFUNDI 

Sasa twende kutazama miradi ya wanafunzi. Kwanza mradi wa meko na vyombo vya udongo kama vile vyungu. Kuna aina mbili za meko. Meko ya mkaa na meko ya kuni. Lengo la mradi huu ni kuwafundisha wanawake matumizi ya meko. Meko ya mkaa yanatumia mkaa kidogo. Pia meko ya kuni yanatumia kuni kidogo. Kama wanawake wa vijijini watatumia kuni au mkaa kidogo, watasaidia kuhifadhi mazingira.

Kwa sasa wanavijiji wengi wanakata miti mingi kutengeneza mkaa au kupata kuni za kupikia. Hapa wanafunzi wanajifunza namna ya kutengeneza meko ya mkaa. Hapa wanafunzi wanajifunza namna ya kutengeneza meko ya kuni. Baada ya kutengeneza meko haya, wananyunyizia majivu ili kuyaimarisha.

© African Studies Institute, University of Georgia.