Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 10: Michezo ya mpira > Lesson 1:

    

MCHEZO WA SOKA

Watu hufanya nini wakati wa mapumziko ili kujistarehesha?

Wanaweza kwenda kuwatembelea ndugu na marafiki. Wengine wanakwenda kucheza au kutazama mpira wa miguu uitwao soka. Mchezo wa soka ni mchezo mashuhuri katika sehemu nyingi za Afrika. Umaarufu wake ni sawa sawa na mchezo wa mpira wa miguu au vikapu Amerika au ragbi huko Uingereza, Australia na Afrika ya kusini.

Hizi ni timu mbili za mjini Morogoro. Wanajiandaa kwa mashindano.

Je Wanafanya nini sasa?

Je, Wanafanya mazoezi ya mwili. Wanaruka ruka na wananyoosha viungo vya mwili. Sasa mashindano ya soka yanaanza. Timu moja imevalia jezi za bluu na nyeupe. Timu ya pili imevalia jezi nyekundu na nyeupe.

© African Studies Institute, University of Georgia.