Home
Overview
Technical Help

Select Unit > Unit 10: Michezo ya mpira > Lesson 2:

    

MPIRA WA NETIBOLI

Hizi ni timu tatu za mchezo wa netiboli mjini Morogoro. Wanajiandaa kwa mashindano.

Je wanafanya nini sasa?

Wanafanya mazoezi ya mwili. Wanatembea kwa kasi. Wanaruka ruka, wananyoosha viungo, na wanaizowesha miguu na mikono yao.

Hizi ni timu tatu za netiboli. Timu moja imevalia sare nyekundu na nyeupe. Timu ya pili imevalia sare ya kijani kikavu na nyekundu. Timu ya tatu imevalia sare ya buluu na nyeusi.

Mchezo sasa utaanza. Wachezaji wa timu zote mbili wanatambulishwa kwa mgeni wa heshima.

© African Studies Institute, University of Georgia.