AINA ZA NGOMA
Lugha ni chimbuko la
utamaduni. Utamaduni unazingatia pia
nyimbo
na ngoma za
wenye utamaduni. Nyimbo na ngoma ni sehemu muhimu sana katika utamaduni wa waswahili
na waafrika kwa
ujumla. Huko Unguja kuna aina nyingi za ngoma na nyimbo ambazo zinasisitiza utamaduni
wa wakazi wa
sehemu hii.
Ngoma hizi huchezwa na wanaume na wanawake kama tutakavyoona. Ngoma wanazotumia hutengenezwa
na wenyeji wenyewe.
Hawanunui ngoma zao kutoka nchi za nje. Kabla ya kuanza kuzipiga ngoma hizi wanaziweka
karibu na joto la moto.
Baada ya ngozi kupata joto inavutika na
huwa na mlio mkali zaidi.
Twende tuwatazame wachezaji hawa.
Ngoma hii inaitwa ngoma ya msewe. Huchezwa na wanaume na wanawake. Wanaume huvaa kofia,
shati, na kikoi na
Wanashika fimbo.
Wanawake huvaa gauni na kufunga kanga kiunoni.
Ngoma hizi huchezwa hasa katika sherehe Za kijadi kama vile jando na
katika harusi.
|